Kuelekea siku ya kilele cha Vijana Duniani, Team ya Tanzania Lambert Foundation (TLF) leo tarehe 12 mwezi Agosti 2023 kupitia wawakilishi wao katika kutambua umuhimu na mchango wa vijana katika Taifa la Tanzania na kidunia kwa ujumla, wamekabidhi baadhi ya vifaa vya shule kwa wanafunzi watatu kutoka kituo cha watoto yatima cha Kinondoni Moscow, wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha tano hivi karibuni.

Katika picha ya pamoja Timu ya T.L.F na Mabinti watatu kutoka kushoto Sophia, Mwajuma,na aliyeshika begi Hanifa pamoja na Mlezi wao Bi. Khadija kutoka kituo cha watoto wahitaji MAUNGA katika ofisi za Tanzania Lambert Foundation ( TLF) Kinondoni jijini Dar- es -Salaam.
Wanafunzi hao Hanifa, Mwajuma na Sophia walikabidhiwa vifaa hivyo mbele ya mlezi wao kwenye ofisi za Tanzania Lambert Foundation(TLF) baada ya kuzungumza machache na vijana hao kisha kuwachangia uniform na baadhi ya vifaa vingine vitavyoenda kutumika shuleni kama kati ya kutimiza ahadi yao kwa wanafunzi hao baada ya kufanya vizuri mitihani yao ya kidato cha nne.
